Juventus Yahamia kwa Adeyemi

Klabu ya Juventus imehamishia nguvu kwa winga wa klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani Karim Adeyemi ambaye anatajwa kwenda kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuelekea msimu ujao.

Juventus kwa misimu mitatu wamekua wakipitia wakati mgumu katika ligi kuu ya Italia lakini pia kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya, Hivo mikakati yao ni kuhakikisha wanasajili wachezaji wenye ubora mkubwa kwajili ya kuirudisha heshima ya klabu hiyo ambayo imepotea kwasasa.juventusMchezaji Karim Adeyemi inaelezwa yuko tayari kujiunga na miamba hiyo ya soka kutoka nchini Italia lakini ofa ya kwanza ambayo walituma ilipigwa chini na klabu ya Borussia Dortmund, Hivo kwasasa wanajiandaa kutuma ofa nyingine kwajili ya kuhakikiisha wanakamilisha dili hilo mapema.

Winga Adeyemi anatajwa anakwenda kua mbadala wa Federico Chiesa ambaye kwa muda mwingi ameonekana kuandamwa na majeraha, Lakini pia klabu hiyo pia imemueka sokoni kuelekea msimu ujao hivo ni wazi Adeyemi atakwenda kuchukua nafasi ya winga huyo wa kimataifa wa Italia.

Klabu ya Borussia Dortmund kwasasa wanaisubiri klabu ya Juventus wawezi kutuma ofa ya pili ambayo itakidhi kiwango ambacho wanakihitaji ili kumuachia mchezaji huyo, Kwani mchezaji huyo ameonesha ana nia ya kujiunga na vibibi vizee vya Turin kueleka msimu wa 2024/25.

Acha ujumbe