Juventus Mawindoni kwa Sancho

Klabu ya Juventus inaelezwa iko kwenye mawindo ya kumnasa winga wa klabu ya Manchester United Jadon Sancho kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa mwezi huu.

Klabu ya Juventus mpaka sasa inafanya mazungumzo na wakala wa winga Sancho kwajili ya kumshawishi kujiunga na miamba hiyo ya soka kutoka nchini Italia, Mustakabli wa winga huyo wa kimataifa wa Uingereza ndani ya klabu ya Man United bado upo wazi kwakua klabu hiyo bado ipo kwenye mpango wa kumuuza winga huyo.juventusWinga Jadon Sancho licha ya kumaliza tofauti zake na kocha Eric Ten Hag lakini bado klabu ya Man United inaelezwa ipo kwenye mchakato wa kumuuza winga huyo, Lakini haitamuuza tu itazingatia ofa nzuri ambayo itakuja mezani ili waweze kumuachia hivo miamba hiyo ya soka kutoka Italia inasubiriwa ipeleke ofa rasmi.

Vyanzo mbalimbali kutoka nchini Italia vinaeleza kua Juventus wanataka kumchukua Sancho kwa mkopo wa msimu mzima ambao utakua na kipengele cha kumnunua, Hivo kilichobaki ni Man United kukubaliana na mpango huo ikielezwa pia winga huyo wa zamani wa Dortmund yupo tayari kutimka klabuni hapo.

Acha ujumbe