Juventus Bado Wanataka Kumuuza Chiesa

Klabu ya Juventus bado imeshikilia msimamo wake wa kutaka kumuuza winga wake matata ndani ya klabu hiyo raia wa kimataifa wa Italia Federico Chiesa.

Kocha wa klabu ya Juventus Thiago Motta amezungumza na kusema kua mpaka sasa Chiesa ni mchezaji wa Juventus, Lakini hakuna kilichobadilika kwenye mipango ya miamba hiyo ya soka kutoka nchini Italia ambapo mpango wao mkubwa ni kumpiga bei winga huyo hatari.juventusChiesa amekua mchezaji ambaye amekua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara jambo ambalo limewafanya klabu ya Juventus kufikiria kumuuza mchezaji huyo, Klabu hiyo imemuweka sokoni Chiesa kwa bei ambayo ni ndogo kulinganisha na namna mchezaji huyo anavyothaminika hii ikonesha wazi Juventus wamedhamiria kumuuza.

Klabu ya Juventus inataka kutengeneza hela kwa kuuza baadhi ya wachezaji ambao hawako kwenye mipango ya klabu hiyo siku za mbeleni, Huku hela hizo zikitumika kununua wachezaji wengine wapya ambao watatumika kutengeneza Juventus mpya ambayo itarejesha ushindani nchini Italia na barani ulaya kwa ujumla.

Acha ujumbe