Juventus Mbioni Kumbeba Thiago Motta

Klabu ya Juventus inayoshiriki ligi kuu nchini Italia iko mbioni kumalizana na kocha wa klabu ya Bologna raia wa kimataifa wa Italia Thiago Motta kuelekea msimu ujao.

Juventus baada ya kuachana na kocha wao wa muda mrefu Massimiliano Allegri sasa macho yote wameyaelekeza kwa kocha Thiago Motta ambaye amekua akifanya vizuri ndani ya klabu ya Bologna msimu huu.juventusKocha Thiago Motta amekua kwenye kiwango bora sana na klabu yake ya Atalanta akifanikiwa kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Italia na kuiwezesha timu hiyo kufuzu ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao.

Miamba ya Turin imekua haipo kwenye kiwango bora kwa misimu takribani minne sasa tangu wawe mabingwa mwaka 2020, Hivo wanataka kurudisha ufalme wao kunako ligi kuu ya Italia jambo limewafanya kumuona Thiago Motta kama mtu sahihi wa kufanikisha hilo.juventusTaarifa mpaka sasa kutoka nchini Italia zinaelezwa mazungumzo yamefikia pazuri baina ya kocha Thiago Motta na klabu ya Juventus, Hivo ni wazi inawezekana muda wowote klabu hiyo ikatangaza kumalizana na kocha huyo mchezaji wa zamani wa vilabu vya Inter Milan, Barca, na PSG.

Acha ujumbe