Juventus imethibitisha kuwa Khephren Thuram alifanyiwa upasuaji wa goti mjini Lyon Alhamisi asubuhi, huku Juan Cabal akipata jeraha tofauti la misuli wakati wa mazoezi.

Kwa mujibu wa taarifa ya kitabibu iliyotolewa na klabu hiyo, Thuram alifanyiwa upasuaji wa chondroplasty kwa ajili ya kutibu tatizo la cartilage kwenye sehemu ya kneecap (patella) ya goti lake la kulia.
Upasuaji huo ulifanywa na Dk. Bertrand Sonnery-Cottet katika Hospitali ya Privé Jean Mermoz mjini Lyon, huku Mkuu wa Kitengo cha Tiba cha Juventus, Dk. Luca Stefanini, akiwa pia amehudhuria.
Klabu hiyo imesema upasuaji huo umefanikiwa kikamilifu na kwamba kiungo huyo ataanza programu yake ya kujiuguza kuanzia Ijumaa. Hakuna muda rasmi uliotolewa wa kurejea uwanjani, ingawa Tuttosport iliripoti kwenye ukurasa wake wa mbele wa Alhamisi kwamba Thuram anaweza kukaa nje kwa muda usiopungua miezi minne.
Beki huyo wa Colombia alilalamika kupata tatizo la misuli wakati wa mazoezi ya Jumatano na kufanyiwa vipimo vya picha katika kituo cha J Medical Alhamisi asubuhi. Vipimo hivyo vilibaini jeraha dogo kwenye misuli ya semimembranosus katika paja lake la kushoto.


