Juventus Yakataa Ombi la Nottingham Forest kwa Gatti

Kulingana na gazeti la Tuttosport, Juventus ilikataa ofa ya €25m kutoka Nottingham Forest kwa Federico Gatti mwezi Agosti.

 

Beki huyo wa Kiitaliano alifunga bao la ushindi dakika za lala salama katika ushindi wa 2-1 wa Juventus dhidi ya Monza siku ya Ijumaa, na kumsaidia Bibi Mzee huyo kurejea kileleni kwenye msimamo akisubiri mechi ya leo usiku kati ya Napoli na Inter kwenye Uwanja wa Stadio Maradona.

Bila kusahau kuwa, Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Kulingana na ripoti hiyo, Massimiliano Allegri alizuia kuondoka kwa Gatti baada ya ziara ya maandalizi ya msimu nchini Marekani, ambapo beki huyo wa zamani wa Frosinone alimvutia bosi wa Juventus.

Gatti mwenye miaka 25, amekuwa akianza mara kwa mara kwenye Uwanja wa Allianz msimu huu akiwa na mechi 12 za Serie A na mabao mawili.

Aliitwa na kocha wa Italia Luciano Spalletti mnamo Oktoba na Novemba. Gatti alicheza mechi yake ya kwanza ya Italia chini ya Roberto Mancini katika sare ya 0-0 dhidi ya Uingereza mnamo 2022.

Pia Meridianbet wanakwambia hivi, tembelea maduka yao ya ubashiri uweze kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.

Beki huyo wa Italia alijiunga na Bibi Kizee kutoka Frosinone mwaka 2022 na amecheza mechi 39 akiwa na Juventus. Hivi majuzi ametia saini nyongeza ya kandarasi kwenye Uwanja wa Allianz hivyo mkataba wake wa sasa utakamilika Juni 2028.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.