Winga wa Napoli Khvicha Kvaratskhelia atakosa mchezo wao wa leo dhidi ya Atalanta inayoshika nafasi ya pili  kwa sababu ya tatizo la mgongo ambalo litamfanya apumzike kujiangalia hali yake.

 

Khvicha Kvaratskhelia Kuikosa Atalanta Leo

Mchezaji  huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa na kiwango cha kusisimua tangu ajiunge na Napoli kutoka Dinamo Batumi mwezi Julai, akicheza jukumu muhimu katika timu yake inayoongoza ligi kuu ya Italia na kuongoza kundi lao la Ligi ya Mabingwa.

Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Gerogia ana mabao nane na asisti nane katika michezo 17 katika mashindano yote, Kvaratskhelia hajaiweka vibaya timu ya Luciano Spalletti.

Hii imekuwa wiki ngumu ingawa, huku mbio za ushindi za Napoli za michezo 13 zikikamilika walipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Liverpool siku ya Jumanne kwenye mchezo wao wa mwisho wa makundi ingawa mabao ya Majogoo yalifungwa baada ya Kvaratskhelia kutolewa nje.

Khvicha Kvaratskhelia Kuikosa Atalanta Leo

Gazzetta dello Sport liliripoti kwamba Khvicha alivamiwa nyumbani kwake Jumatano usiku, na gari lake aina ya Mini kuibiwa na baadaye kupatikana na polisi.

Sasa kinda huyo atakosa angalau mchezo mmoja, huku Napoli wakisema kwenye tovuti yao: “Khvicha Kvaratskhelia hatashiriki katika safari yao ya kuwafuata Atalanta baada ya kusumbuliwa na maumivu makali ya kiuno.”

Lakini  inaonekana anaweza kurejea kwa ajili ya mchezo wa Jumanne dhidi ya Empoli, au Jumamosi inayofuata dhidi ya Udinese, mechi zote mbili zitakazopigwa kwenye Uwanja wa Stadio Diego Armando Maradona.

Khvicha Kvaratskhelia Kuikosa Atalanta Leo

Hiyo ndiyo imekuwa athari ya Khvicha huko Napoli, amefananishwa na gwiji wa klabu Maradona, akipata jina la utani ‘Kvaradona’. Mshambuliaji wa Argentina Maradona ndiye aliyekuwa msukumo wa Napoli wakati klabu ya Naples iliposhinda mataji ya Serie A 1986-87 na 1989-90 ambao ndio ushindi wao pekee wa Scudetto hadi sasa.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa