Kiungo wa Kati wa Fiorentina, Bove Azungumza Baada ya Kuanguka Uwanjani

Kiungo wa Fiorentina, Edoardo Bove, amekuwa macho na anazungumza baada ya kutumia usiku mzima kwenye huduma ya dharura, kufuatia ajali ya kutisha uwanjani wakati wa mechi ya Serie A kati ya Fiorentina na Inter Jumapili usiku.

Kiungo wa Kati wa Fiorentina, Bove Azungumza Baada ya Kuanguka Uwanjani

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa gazeti la La Repubblica toleo la Firenze, Bove mwenye umri wa miaka 22 amekuwa macho na tayari haipo tena kwenye mashine ya kupumulia.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

“Nashukuru kila mtu,” ndivyo alivyosema kwa maneno yake ya kwanza baada ya kuamka, kulingana na taarifa ya asubuhi ya Jumatatu.

Mechi kati ya Fiorentina na Inter iliahirishwa katika dakika ya 17 baada ya Bove kuanguka akiwa uwanjani na alikimbizwa haraka kwa ambulance kando ya uwanja.

Kiungo wa Kati wa Fiorentina, Bove Azungumza Baada ya Kuanguka Uwanjani

Sky Sport Italia iliripoti kwamba mchezaji huyo wa zamani wa akademi ya Roma alikuwa anapumua kiasili alipopelekwa kwenye ambulance na kwamba alirejea fahamu akiwa hospitali ya Careggi karibu na Stadio Artemio Franchi jioni hiyo.

Lega Serie A ilithibitisha kwamba mechi hiyo ilisitishwa na haitaendelea Jumapili jioni. Itakapopangwa tena, mchezo utaendelea kutoka dakika ya 17.

Acha ujumbe