Lautaro Martinez Mbioni Kusaini Mkataba Mpya Inter

Mshambuliaji na nahodha wa klabu ya Inter Milan mabingwa wa ligi kuu nchini Italia Lautaro Martinez yuko mbioni kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia wababe hao wa soka kutoka nchini Italia.

Lautaro Martinez amekua na mazungumzo na klabu ya Inter Milan kwa muda sasa wakijadili namna klabu hiyo inavyoweza kumuongezea mkataba na kuboresha maslahi yake, Rais wa klabu hiyo bwana Marotta wakati akiongea na waandishi wa habari amewahakikishia kua mchezaji huyo yuko mbioni kuongeza kandarasi.lautaro martinezMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina ambaye ameiongoza klabu hiyo kutwaa taji la ligi kuu ya Italia mara mbili amekua moja ya wachezaji muhimu sana ndani ya kikosi cha Nezzazuri, Jmabo ambalo limewavutia mabosi wa klabu hiyo kumuongezea mkataba mpaya aendelee kuwepo klabuni hapo zaidi.

Mshambuliaji Lautaro Martinez amekua akifukuziwa na vilabu kadhaa barani ulaya wakihitaji saini yake kwa takribani misimu mitatu sasa, Lakini klabu ya Inter Milan walikomaa na kushindwa kumuachia mchezaji ambaye amekua mhimili mkubwa sana ndani ya klabu hiyo.

Acha ujumbe