Klabu ya Lazio inayoshiriki ligi kuu nchini Italia maarugu kama Serie A kupitia rais wake Claudio Lotito amesisitiza kiungo wa klabu hiyo raia wa Serbia Sergej Milinkovic Savic hauzwi kwenda klabu yeyote.

Kiungo huyo ambaye anajiandaa kuiwakilisha timu yake ya taifa ya Serbia kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar amekua akihusishwa kwa muda mrefu kutaka kutimka katika klabu hiyo licha ya kushindikana kwa usajili huo.lazioRais wa klabu ya Lazio ameendelea kuweka bayana kua mchezaji huyo hauzwi na hakuna majadiliano yeyote ya kumuuza mchezaji huyo yamefanyika mpaka wakati huu, licha ya tetesi kua nyingi kudai kiungo huyo atatimka kloabuni hapo.

Klabu ya Manchester United imekua ikihusishwa na kiungo huyo mwenye miaka 27 kwa muda mrefu ila kwasasa klabu ya Juventus chini ya kocha Massimiliano Allegri wanaonekana kua mstari wa mbele kuhitaji huduma ya Savic.lazioLakini msimamo wa klabu ya Lazio wakiongozwa na rais wao Claudio Lotito anaeleza mchezaji huyo hatauzwa na cha zaidi wako kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa