Locatelli: Sijutii Kutojiunga Arsenal

Kiungo wa klabu ya Juventus Manuel Locatelli amebainisha kua hajutii kujiunga na klabu ya Juventus na kutojiunga na washika mitutu kutoka jiji la london klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Italia amefanya mazungumzo na kituo kimoja nchini Italia na kuweka wazi suala hilo ikumbukwe kiungo huyo alifuatiliwa kwa karibu sana na klabu ya Arsenal miaka miwili nyuma na dili lilikaribia kukamilika, Lakini haikufanikiwa na kiungo huyo kujiunga na klabu ya Juventus ya nchini kwao Italia.locatelli

“Sijutii kujiunga na Juventus badala ya Arsenal.”

“Lakini napenda kuangalia soka, na napenda kuangalia mechi zao na namheshimu kocha wao, Mikel Arteta.”

Kiungo Locatelli alijiunga na wababe hao wa soka nchini Italia msimu uliopita kwa uhamisho wa kudumu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mzima akitokea klabu ya Sassuolo, Mchezaji huyo amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu ya Juventus tangu alipojiunga na miamba hiyo ya soka nchini Italia.

Acha ujumbe