Nyota kutoka Ubelgiji, Romelu Lukaku, ameweka wazi kuwa bado ana mapenzi makubwa na Napoli licha ya msimu mgumu uliogubikwa na majeraha, migogoro ya ndani na maneno mengi kutoka kwenye vyombo vya habari. Lukaku amesema taarifa zilizoenea kuhusu kutokuwepo kwake kambini ziliongezewa chumvi kupita kiasi, huku akisisitiza kuwa lengo lake lilikuwa kurejea akiwa fiti zaidi uwanjani.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 33 alikiri kukerwa na namna baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti safari yake ya kwenda Ubelgiji kwa ajili ya matibabu ya majeraha ya misuli ya paja. Kwa mujibu wa Lukaku, watu wengi walidhani alikuwa ameikimbia timu, lakini ukweli ni kwamba alikuwa akijitahidi kurudi kwenye kiwango chake bora haraka iwezekanavyo. “Sikuenda Ubelgiji kwa mapumziko, nilikuwa natafuta njia ya kurudi kuwa bora zaidi,” alisema kwa msisitizo.
Msimu wa 2025/26 haukuwa rahisi kwa Lukaku ndani ya Napoli. Alipata nafasi ndogo ya kucheza Serie A na mara nyingi aliingia kama mchezaji wa akiba kutokana na majeraha yaliyomsumbua kwa muda mrefu. Hali hiyo ilizua mvutano kati yake na uongozi wa klabu pamoja na kocha Antonio Conte, ambaye alionyesha kutofurahishwa na kutopata taarifa moja kwa moja kutoka kwa mchezaji huyo kuhusu maendeleo ya matibabu yake.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Licha ya Conte kuthibitisha kuondoka Napoli mwishoni mwa msimu huu, Lukaku amesema hana mpango wowote wa kuondoka klabuni hapo. Straika huyo bado ana mkataba hadi mwaka 2027 na ameweka wazi kuwa yeye si aina ya wachezaji wanaolazimisha kuuzwa wanapokutana na changamoto. Kauli hiyo imewapa matumaini mashabiki wa Napoli wanaotaka kumuona akirejea kwenye ubora wake msimu ujao.

Wakati wengi wakijiuliza kama bado ana uwezo wa kucheza kwenye kiwango kikubwa, timu ya taifa ya Ubelgiji imeendelea kumuamini nyota huyo na imemjumuisha kwenye kikosi cha Kombe la Dunia. Ubelgiji itaanza kampeni yake dhidi ya Misri Juni 15 kabla ya kukutana na Iran na New Zealand katika hatua ya makundi.



