Lukaku Arejea Napoli, Atoa Tumaini Timu ya Taifa ya Ubelgiji

Mshambuliaji wa Napoli, Romelu Lukaku, anatarajiwa kurejea kikosini rasmi, hatua inayotajwa kuongeza matumaini kwa timu ya taifa ya Ubelgiji kuelekea mashindano ya FIFA World Cup mwezi ujao.

Lukaku Arejea Napoli, Atoa Tumaini Timu ya Taifa ya Ubelgiji Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Italia, Lukaku amerejea Napoli baada ya kukaa kwa wiki tano nchini Ubelgiji akipatiwa matibabu ya majeraha ya muda mrefu. Hata hivyo, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alitozwa faini na klabu hiyo baada ya kushindwa kurejea mara baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa mwezi Machi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Inaelezwa kuwa Lukaku alichagua kubaki Ubelgiji ili kuendelea na matibabu chini ya mtaalamu wake binafsi wa viungo, jambo lililosababisha Napoli kumkata asilimia 20 ya mshahara wake wa mwezi. Baadaye alirejea klabuni Aprili 20, lakini akarudishiwa ruhusa ya kuendelea na matibabu nje ya Italia.

Lukaku Arejea Napoli, Atoa Tumaini Timu ya Taifa ya Ubelgiji Kocha wa Napoli, Antonio Conte, alionesha kutoridhishwa na mwenendo wa mchezaji huyo akisema “Sikupata nafasi ya kuzungumza naye. Najua mmoja wa viongozi wetu alizungumza naye, lakini hakukuwa na mawasiliano ya moja kwa moja kati yetu.”

Lukaku Arejea Napoli, Atoa Tumaini Timu ya Taifa ya Ubelgiji Conte aliongeza kwa masikitiko “Alifika katika kituo cha mazoezi, lakini hakuna aliyegonga mlango wa ofisi yangu. Hilo liliniumiza, nilitegemea hata salamu au ujumbe wowote. Katika hali kama hizi, kocha hujaribu kuelewa kila mtu, lakini hakuna anayejitahidi kumuelewa kocha.”

Lukaku Arejea Napoli, Atoa Tumaini Timu ya Taifa ya Ubelgiji Licha ya changamoto hizo, kurejea kwa Lukaku kunakuja wakati muhimu kwa Napoli ambao wako nafasi ya pili katika Serie A, huku wakiwa na michezo mitatu iliyosalia msimu huu. Kwa upande wa timu ya taifa ya Belgium, Lukaku tayari amefunga mabao 89 katika mechi 124, na anatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Misri, Iran na New Zealand katika Kundi G la Kombe la Dunia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.