Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Inter Milan, na Man United Romelu Lukaku ni kama amezaliwa upya akiwa na klabu ya As Roma kwani anaonesha ubora mkubwa akiwa ndani ya timu hiyo.
Lukaku amefanikiwa kufunga mabao mawili leo kwa mara nyingine akiihakikishia klabu ya As Roma kupata alama tatu muhimu katika mchezo wa leo wa ligi kuu ya Italia dhidi ya klabu ya Cagliari.Klabu ya As Roma ilikua ugenini leo kukipiga dhidi ya Cagliari na mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Ubelgiji akifanikiwa kufunga mabao mawili ambayo yalichangia Roma kushinda jumla ya mabao manne kwa moja.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ameshafanikiwa kufunga mabao saba katika michezo yake nane ya mwisho akiwa na klabu yake mpya ya As Roma hii inaonesha kua mshambuliaji huyo ameanza kurudisha makali yake.Romelu Lukaku amekua akionesha ubora mkubwa tangu atue ndani ya klabu ya As Roma kwani klabu hiyo haikufanikiwa kuanza msimu vizuri, Lakini mshambuliaji huyo alikua anaonesha ubora hata kwenye michezo ambayo klabu yake imepoteza.