Maldini: "Milan Lazima Wawe na Tamaa Zaidi"

Mkurugenzi wa AC Milan na gwiji wa klabu hiyo Paolo Maldini amesema kuwa lazima wawe na malengo zaidi na wanalenga kushinda zaidi taji la Serie A msimu huu.

 

Maldini: "Milan Lazima Wawe na Tamaa Zaidi"

The Rossoneri walishinda Scudetto msimu uliopita kwa mara ya kwanza tangu kampeni za 2010-11 baada ya kuilaza Sassuolo 3-0 katika siku ya mwisho, wakipigania kombe kutoka kwa wapinzani wao Inter.

Juhudi za Milan kunyanyua taji la Serie A kwa msimu wa pili mfululizo zimewafanya kushinda mechi 10 kati ya 15 za mwanzo, hata hivyo licha ya kushika nafasi ya pili kwenye msimamo huku vinara Napoli bado hawajapoteza mchezo woowte na tayari wanaongoza kwa pointi 8 dhidi ya vijana wa Stefano Pioli.

Milan imefanya vyema barani Ulaya, hata hivyo, na kuifanya kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2013-14.

Maldini: "Milan Lazima Wawe na Tamaa Zaidi"

Maldini, ambaye alishinda mataji saba ya Serie A na mataji matano ya Ligi ya Mabingwa akiwa na Rossoneri kama mchezaji, anahisi wanapaswa kutafuta mafanikio ya bara ili kuongeza ushindi wao wa nyumbani msimu uliopita.

Maldini aliiambia MilanTV: “Mechi iliyochezwa Sassuolo kunyakua taji siku ya mwisho ilimaliza kipindi cha miaka mitatu ambacho kilianza 2019 kwa mradi mahususi, ambao haukutarajia ushindi wa Scudetto, lakini walitarajia kurudi kuwa na ushindani.”

Maldini hakuishia hapo aliongeza kwa kusema kuwa kwakweli wanazungumza juu ya Milan, na hawawezi kuridhika na kushinda taji la Serie A, lazima wawe na hamu zaidi. Wanaweza na lazima wawe wahusika wakuu katika mashindano manne ambayo yamesalia.

Maldini: "Milan Lazima Wawe na Tamaa Zaidi"

Michuano ya Kombe la Dunia imeshuhudia wachezaji kadhaa wa Milan wakichukua jukumu la kuingiza timu zao za Taifa nchini Qatar. Wafaransa Theo Hernandez na Olivier Giroud wanatazamiwa kucheza fainali siku ya Jumapili dhidi ya Argentina.

Hernandez alifunga katika ushindi wa nusu fainali dhidi ya Morocco na Giroud amekuwa mfungaji bora wa muda wote wa Les Bleus, huku winga Rafael Leao pia akiifungia Ureno mara mbili.

Maldini: "Milan Lazima Wawe na Tamaa Zaidi"

Mkurugenzi huo alimzungumzia Raphael Leao na kusema alifanya jukumu lake, mabao mawili katika Kombe la Dunia si jambo dogo, kwa bahati mbaya hakucheza sana lakini anadhani bado ilikuwa uzoefu mzuri na wa hali ya juu kwake.

Olivier na Theo wamekuwa nyota tangu mwanzo, na wanajivunia kuwaona kwenye kikosi cha kwanza wakiwa wamefika fainali ya Kombe la Dunia.

Maldini: "Milan Lazima Wawe na Tamaa Zaidi"

Milan itarejea kwenye hatua ya ushindani Januari 4, watakapomenyana na Salernitana kwenye Serie A.

Acha ujumbe