Mazzarri Ana Rekodi Mbaya Zaidi ya Napoli Kuliko Rudi Garcia

Walter Mazzarri yuko mbioni kutimuliwa na Napoli akiwa amekusanya pointi chache kuliko Rudi Garcia katika mechi 12 za Serie A.

Mazzarri Ana Rekodi Mbaya Zaidi ya Napoli Kuliko Rudi Garcia

Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis anatazamiwa kukutana na Francesco Calzona leo na huenda akamuweka chini ya mkataba msaidizi wa zamani wa Maurizio Sarri na Luciano Spalletti kuchukua nafasi ya Mazzarri hadi mwisho wa msimu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Mkufunzi huyo wa Tuscan amekusanya pointi 15 pekee katika mechi 12 za Serie A tangu kuchukua nafasi ya Rudi Garcia mwezi Januari.

Mfaransa huyo alikuwa amepata pointi 21 katika mechi 12 za mwanzo msimu huu na alitimuliwa wakati Partenopei inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Serie A, huku sasa ikiwa nafasi ya 9, nje ya msururu wa ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mazzarri Ana Rekodi Mbaya Zaidi ya Napoli Kuliko Rudi Garcia

Mazzarri ameshinda michezo minne ya Serie A, akapoteza mitano na kutoka sare mara tatu ikiwemo sare ya 1-1 Jumamosi dhidi ya Genoa kwenye Uwanja wa Stadio Maradona.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Napoli watawakaribisha Barcelona katika mechi ya mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumatano, lakini Mazzarri huenda asiwe kwenye dimba la Partenopei ndani ya siku mbili.

 

Acha ujumbe