Mourinho Atupa Dongo Man City

Kocha wa klabu ya As Roma Jose Mourinho ametupa dongo kwa klabu ya Manchester City juu ya kiungo raia wa kimataifa wa Uingereza anayekipiga klabuni hapo Kalvin Phillips.

Jose Mourinho amesema hataki kuonekana kama ana wivu lakini unaweza kutazama klabu ya Manchester City walimsajili kiungo Kalvin Phillips kwa €milioni 80 lakini wanamuachia aondoke klabuni hapo kwasasa kwakua amekosa nafasi klabuni hapo.mourinhoKocha huyo wa zamani wa vilabu vya Chelsea, Real Madrid, na Manchester United ameeleza kua wakati Manchester City wanafanya hayo, Klabu yake ya As Roma ni vigumu kusajili hata mchezaji mmoja.

Kauli hii imeonekana kama dongo kwa Man City na mpinzani wake wa muda mrefu kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola, Kwani Jose anataka kuonesha kua ni rahisi kw aklabu hiyo na kocha Guardiola kwakua wanatumia hela nyingi kupata wachezaji wazuri na wakifeli pia wanapata wengine.mourinhoKocha Jose Mourinho kutokana na kauli ambayo ameieleza ni wazi anaonesha kua Manchester City wanaweza kupata mafanikio kwa wepesi kutokana na namna wanatumia pesa na wanapata mchezaji yeyote wanayemtaka tofauti na vilabu vingine.

Acha ujumbe