Kocha mkuu wa AS Roma Jose Mourinho amesikitika kukosekana kwa Paulo Dybala baada ya Roma kupokea kichapo cha 1-0 dhidi ya Lazio, lakini akaweka wazi kuwa mchezaji huyo wa Kimataifa wa Argentina atarejea kabla ya Kombe la Dunia.

 

Mourinho Anasikitika Kukosekana kwa Dybala Baada ya Kichapo Jana

Dybala amekosekana tangu Oktoba 9 baada ya kupata jeraha la msuli wa paja, lakini Mourinho anatumai kuwa atarejea dhidi ya Torino Jumapili ijayo, jambo ambalo pia litakuwa ni nguvu kwa Argentina kabla ya safari yao ya Qatar.

Vijana wa Mourinho walikuwa nyumbani walipopoteza dhidi ya Lazio, ambapo bao hilo lilifungwa na Felipe Anderson katika dakika ya 29 na ndilo ambalo lililala mpaka mpira kumalizika.

Mourinho Anasikitika Kukosekana kwa Dybala Baada ya Kichapo Jana

Kocha huyo alisema kuwa; “Ni wazi anataka kwenda Kombe la Dunia, ni vigumu kukataa hilo na ikiwa kuna mabadiliko mazuri ya jeraha lake, tunatumai kuwa atarejea Jumapili dhidi ya Torino.”

Pia aliulizwa kuhusu rekodi yao mbaya ya kupoteza dhidi ya Lazio na Napoli wakiwa nyumbani akasema kuwa Roma walipoteza michezo hiyo miwili mfululizo kwakuwa hawakustahili

Mourinho Anasikitika Kukosekana kwa Dybala Baada ya Kichapo Jana

Baada ya kudondosha alama jana Roma wapo katika nafasi ya 6 wakiwa na pointi 25 sawa na Juventus lakini tofauti yao ikiwa ni magoli ya kufungwa na kufunga. Mchezo ujao watakipiga dhidi ya Sassuolo ugenini.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa