Klabu ya Napoli inafikiria kumfuta kazi kocha wake wasasa Rudi Garcia kutokana na kutofurahishwa na mwenendo wake siku za karibuni katika michuano ambayo klabu hiyo inashiriki.
Kipigo walichokipata leo Napoli kutoka kwa Empoli katika dimba lao la nyumbani la Diego Armando Maradona kinaelezwa kuchochoea uongozi wa klabu hiyo kufikiria kumtimua kocha wao Rudi Garcia.Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Italia wamekua hawana muendelezo wa matokeo bora kiwanjani kama ambavyo walionesha msimu uliomalizika, Jambo ambao limekua haliwafurahishi mabosi wa klabu hiyo ikiwemo rais wao Auriello De Laurentiis.
Leo klabu hiyo imepokea kipigo chake cha tatu kunako ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie baada ya michezo 12 kuchezwa, Wakati msimu uliomalizika katika michezo hiyo walikua hawajapoteza mchezo wowote.Uongozi wa klabu ya Napoli unafanya majadiliano ya ndani kujadili ni kocha gabi anawafaa kuchukua nafasi ya Rudi Garcia, Kwani kocha huyo alishaingia kwenye hatari ya kufukuzwa mwezi mmoja nyuma na sasa yuko kwenye hatari hii inawezekana awamu hii wakumuondoa kweli.