Klabu ya soka ya Napoli inayoshiriki ligi kuu nchini Italia inafiikiria kumuongeza mkataba kocha wake wa sasa Luciano Spaletti kutokana na namna ambayo anaiongoza klabu hiyo. Spaletti amefanikiwa kuitengeneza klabu hiyo kua miongoni mwa timu tishio kwenye ligi ya Italia na ulaya kwa ujumla.

Akifanya mahojiano na waandishi wa habari mkurugenzi wa klabu hiyo Cristiano Giuntoli ameeeleza nia yao ya dhati ya kutaka kumuongezea mkataba kocha huyo ili aendelee kusalia kwenye viunga vya Diego Armando Maradonna kutokana na kazi anayoifanya klabuni hapo.napoliLuciano Spaletti amefanikiwa kuifanya klabu ya Napoli kufanya vizuri baada ya nuda mrefu kusuasua baada ya kuondoka kocha maurizio Sarri, Lakini tangu amepewa timu hiyo kocha huyo ameitenegeneza kwa muda mfupi na imeanza kuonesha matunda.

Uongozi wa klabu hiyo unamuona kocha huyo kama nyenzo muhimu ya mradi wao siku za mbeleni hivo wanahitaji kocha huyo aendelee kubaki klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi.napoliKlabu ya Napoli chini ya Spaletti mpaka sasa hivi imepoteza mchezo mmoja kwenye michuno yote lakini katika ligi kuu ya Serie A haijafanikiwa kupoteza mchezo hata mmoja huku wakiwa vinara wa ligi hiyo na kuonesha ni kwa namna gani kocha huyo anafanya kazi kubwa.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa