Kuna habari mbaya kwa Napoli baada ya klabu hiyo kutangaza kuwa Alessandro Buongiorno atakosa maandalizi ya msimu mpya kutokana na jeraha la goti, huku pia akitajwa kuwa huenda akahitaji kufanyiwa upasuaji ambao unaweza kumuweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.




