Kocha wa klabu ya Ac Milan Stefano Pioli amekataa kuhusisha kipigi walichokipokea jana katika mchezo wa ligi kuu ya Italia dhidi ya Fiorentina na mchezo wao unaofuata wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Tottenham.

Kocha Pioli amekua muwazi na kusema wamstahili kupoteza katika mchezo wa jana na hawawezi kutumia mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Tottenham utakaopigwa jijini London kama kisingizio na kocha huyo akiweka wazi kua walistahili kupoteza mchezo huo.PioliKlabu ya Ac Milan watavaana na klabu ya Tottenham katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya 16 bora utakaopigwa katika dimba la Tottenham, Huku klabu ya Ac Milan wakiwa na faida ya bao moja ambalo walishinda wiki mbili nyumba wakiwa nyumbani katika dimba la San Siro.

Kocha Pioli alizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo na kusema hawajapoteza mchezo huo kwasabbu walikua tayari wanaifikiria Tottenham, Lakini wamepoteza mchezo huo kwasababu Fiorentina walicheza vizuri kuliko wao na ni mchezo ambao walistahili kupoteza kwa namna walivyocheza.PioliKlabu ya Ac Milan itakua kwenye hatihati kutoka kwenye nafasi nne za juu kama klabu ya As Roma watafanikiwa kuifunga Juventus leo na kua sawa kwa alama, Huku tofauti ya magoli itawafanya klabu ya As Roma kua juu kwani mpaka sasa vijana wa Jose Mourinho wanalingana magoli na Ac Milan.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa