Kocha wa klabu ya Ac Milan Stefano Pioli ameitaka klabu yake kuhakikisha inapungaza pengo la alama dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Serie A klabu ya Napoli.

Klabu ya Ac Milan ambao ndo mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Serie A mpaka sasa wako nyuma kwa alama tatu dhidi ya vinara Napoli wenye alama 29 huku Milan wao wakiwa na alama 28.pioliAc Milan ambao wamepoteza mchezo dhidi ya Napoli tu, Kocha Pioli yeye anataka klabu hiyo ihakikishe wanapunguza alama walizoachwa na klabu huku kocha wa klabu hiyo akiamini vijana wake wanaweza kufanya ambayo anayafikiria.

Ameyazungumza hayo kocha Pioli wakielekea kucheza mchezo wao wikiendi hii dhidi ya klabu ya Torino ambao hawakupata matokeo mazuri dhidi yao msimun uliomalizika. Hivo wanahitaji alama tatu muhimu ili kuepuka kuongeza pengo dhidi ya Napoli.pioliKocha wa Ac Milan yeye aanasema hawazi zaidi kuongoza ligi kabla ya mapumziko ya kombe la dunia, Lakini hofu yake kubwa ni kuwaruhusu Napoli kuongoza kwa alama nyingi zaidi.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa