Kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Pogba amefungiwa kutojihusisha na mchezo wa soka kwa muda wa miaka minne kutokana tuhuma za kutumia dawa za kuongeza nguvu mchezoni.
Tuhuma za kutumia madawa ya kuongeza Paul Pogba alianza kutuhumiwa nazo mwaka jana, Huku tuhuma hizo zikifanyiwa uchunguzi mpaka leo ambapo majibu yametoka yakionesha ni kweli alikua anatumia madawa ya kuongeza nguvu mchezoni.Kiungo huyo ambaye tangu ajiunge na klabu ya Juventus msimu uliomalizika amekua akiandamwa na majeraha kwa kiwango kikubwa, Huku akifanikiwa pia kucheza michezo michache sana ndani ya klabu hiyo mpaka tuhuma hizo zinamkuta.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa ameeleza katika taarifa yake leo aliyoitoa leo baada ya hukumu amekanusha tuhuma hizo, Huku akisema hajawahi kutumia dawa za kuongeza nguvu mchezoni na anatazamia kukata rufaa katika ya rufaaa ya kimichezo (CAS).Paul Pogba atakua nje ya uwanja kwa muda wa miaka minne kwa mahesabu ni kuanzia mwaka huu 2024 mpaka mwaka 2028 kama tu rufaa yake itatupiliwa mbali na CAS, Lakini rufaa yake ikikubalika kuna uwezekano mchezaji huyo kurejea uwanjani mapema.