Kiungo wa klabu ya Juventus raia wa Ufaransa Andrien Rabiot amefunguka juu ya dili lake na klabu ya Manchester United Kuvunjika katika dirisha lililopita majira ya joto.

Wakati dirisha kubwa likikaribia kufungwa klabu ya Manchester United ilikua ikuhusishwa kwa karibu sana kumhitaji kiungo huyo baada ya dili kiungo wa klabu ya Barcelona Frenkie De jong kuonekana limeshindikana klabuni hapo.rabiotBaada ya dili hili kushindikana ndipo klabu hiyuo ilipoamua kumsajili kiungo kutoka klabu ya Real Madrid Carlos Casemiro ilieigharimu timu hiyuo kiasi cha paundi milioni 70 ili kushuka klabuni hapo.

Baada ya dili la Rabiot kuonekana limekufa ndipo kiungo huyo ameweza kufunguka namna ambavyo dili hili limekufa na kudai “Ni kweli nilikua nikitajika na Man United na nilikua na nafasi ya kupata changamoto ya ligi kuu ya Uingereza, Lakini chaguo langu la kwanza ilikua ni kubaki ndani ya Juventus” Akizungumza kiungo huyo na chombo kimoja cha habari nchini Italia.rabiotAndrien Rabiot ambae amewahi kutamba na klabu ya PSG ya nchini Ufaransa kwasasa amekua ni miongoni mwa wachezaji muhimu ndani ya klabu ya Juventus kutokana na uwezo ambao amekua akiuonesha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa