Winga matata raia wa kimataifa wa Ureno Rafael Leao anayekipiga klabu ya Ac Milan inayoshiriki ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A ameweka wazi kua bado yupo sana ndani ya Milan.
Rafael Leo amesema bado yupo ndani ya mkataba na klabu yake ya Ac Milan japo hajajua yapo litakalokuja kutokea mbele, Kutokana na kauli hiyo winga huyo ameoensha wazi bado ataendelea kuwepo klabuni hapo kwani bado ana mkataba na miamba hiyo ya soka nchini Italia.Winga huyo amekua akihusishwa kuondoka ndani ya klabu hiyo mara kwa mara na vilabu kadhaa vikubwa barani ulaya vikihusishwa na saini yake, Lakini mchezaji huyo bado ameendelea kushikilia msimamo wake kua ataendelea kuwepo ndani ya timu hiyo.
Staa huyo wa klabu ya Ac Milan amesema “Milan ni nyumbani kwangu na klabu hii imesaidia kukua na ninafuraha kuwa hapa, nataka kushinda jambo muhimu nikiwa ndani ya timu hii”Kutokana na maneno ya Winga Rafael Leao ni wazi bado anatamani kuendelea kuitumikia klabu ya Ac Milan, Huku vilabu kama Manchester City, Man United, pamoja na Real Madrid ambavyo vinahusishwa na winga huyo vinapaswa kufanya kazi kubwa ili kumg’oa ndani ya Ac Milan.