Klabu ya AS Roma wamelazimika kumkata mchezaji wao mpya Ola Solbakken kwenye kikosi chao cha Ligi ya Europa kutokana na usawa wa matumizi wa timu za Ulaya.
Mshambuliajii huyo wa Norway mwenye umri wa miaka 24 alisaini mkataba wa miaka minne na nusu na Giallorossi mwezi uliopita, akijiunga kwa uhamisho bure baada ya mkataba wake kumalizika na Bodo/Glimt.
Solbakken alijipatia umaarufu barani Ulaya baada ya kufunga mabao matatu katika mechi mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Europa Conference dhidi ya Roma msimu uliopita.
Kama ilivyobainishwa na TMW, UEFA iliwalazimu Roma kumkata mchezaji katika kikosi chao cha Ligi ya Europa baada ya kukagua orodha yao na kugundua kuwa timu hiyo ilivuka mipaka ya gharama iliyokubaliwa, kufuatia adhabu iliyotolewa mwanzoni mwa Septemba 2022.
Kulikuwa na tofauti ya tafsiri katika sheria kati ya klabu na baraza la uongozi, lakini Giallorossi hakutaka kukata rufaa na hivyo kuamua kukata Solbakken ili kusajili kikosi chao.
Roma wangeweza tu kuchagua kupunguza moja ya nyongeza tatu mpya Solbakken, Diego Llorente na Georginio Wijnaldum. Mshambuliaji huyo wa Norway alichaguliwa kwa sababu klabu ilitaka kuhakikisha kuwa ina safu ya ulinzi ya kutosha, na hawakuwa na nia ya kumkata mchezaji huyo wa mkopo wa Paris Saint-Germain.