Ronaldo Atuma Ujumbe Kwa Mrithi Wa Messi!

Mchezaji wa Juventus, Christano Ronaldo ametuma pole na ujumbe wa kumfariji nyota mdogo wa Barcelona, Ansu Fati kufuatia majeraha yake ya goti yanayomkabili.

Ronaldo amekuwa akijulikana kutoa ushauri na motisha kwa watu wengi walio na shida. Katika post aliyetuma CR7 hivi karibuni aliandika maneno ya kumtakia Ansu Fati apone na arudi haraka kwenye michezo.

Ansu Fati alipata majeraha ya goti katika mechi ya mwisho mwezi Novemba akiwa na Barcelona na hajacheza tena mpaka sasa. Katika ripoti iliyotolewa na timu ya madaktari wa Barcelona wanadai kwamba Ansu Fati anaendelea vizuri na anaweza asifanyiwe operesheni ya goti kama ilivyotakiwa mwanzoni.

Ansu Fati amekuwa akidhaniwa kuwa mrithi wa messi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusakata kabumbu, Messi pia katika moja ya mahojiano yake alidai kwamba Ansu Fati ni mchezaji mzuri na anayemkubali sana.

Ronaldo amekuwa akijihusisha na mambo mbalimbali ya kutia moyo watu wanaopitia wakati mgumu katika michezo.

JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

5 Komentara

    Pole sana Fati

    Jibu

    Cr7 amefanya jambo jema sana

    Jibu

    Cr7 yuko vizuri

    Jibu

    Haya buana

    Jibu

    Huo ndo upendo

    Jibu

Acha ujumbe