Kocha Simeone Inzaghi ataendelea kuwepo ndani ya viunga vya San Siro mpaka mwezi Juni 2026 baada ya kufanikiwa kuongeza mkataba wa kuendelea kuwepo klabuni hapo.
Simeone Inzaghi amekubali kuongeza mkataba ndani ya klabu hiyo baada ya mazungumzo ya muda mrefu hatimae amekubaliana na klabu hiyo kuongeza kandarasi ya kuendelea kusalia ndani ya timu hiyo, Hii imekuja baaada ya kazi kubwa iliyotukuka aliyoifanya ndani ya klabu hiyo.Ndani ya misimu mitatu ambayo amekaa ndani ya klabu ya Inter Milan amefanikiwa kuipatia klabu hiyo taji la ligi kuu ya Italia maarufu kama Scudetto, Lakini pia amefanikiwa kuifikisha klabu hiyo kwenye hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya mwaka 2023.
Kocha Simeone Inzaghi atapokea kiasi cha Euro milioni 6.5 kwa mwaka baada ya kuongeza mkataba ndani ya timu hiyo, Huku atapata bonasi ya kiasi cha Euri milioni 2 kama klabu ya Inter Milan itafanikiwa kubeba ligi kuu ya Italia ndani ya misimu mitatu.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.