Thiago Motta Kusaini Juventus Wiki Ijayo

Aliyekua kocha wa klabu ya Bologna Thiago Motta anatarajiwa kusaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Jucentus wiki ijayo baada ya kumalizana na vigogo hao wa soka kutoka nchini Italia.

Klabu ya Juventus imeachana na kocha wake aliyedumu muda mrefu klabuni hapo kwa takribani miaka 9 Massimiliano Allegri baada tu ya kushinda ubingwa wa Coppa Italia, Huku Thiago Motta nyota wa zamani wa vilabu ya Barcelona na PSG akitarajiwa kua kocha mpya wa klabu hiyo.thiago mottaJuventus wako kwenye mchakato wa kuijenga klabu hiyo upya na kuirudisha kwenye ubora ambao imekua nao kwa miaka mingi, Kwani miaka mitatu ya hivi karibuni wameonekana kusuasua kuanzia kwenye ligi ya nyumbani mpaka kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Wababe hao wa soka nchini Italia wanatarajiwa kumsainisha mkataba na kumtangaza kocha huyo wa zamani wa Bologna siku ya Jumanne au Jumatano kutokana na vyanzo mbalimbali vilivyoripoti kutoka nchini Italia, Huku akisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia klabu hiyo kwa maana atasalia klabuni hapo mpaka mwaka 2027.thiago mottaKocha Thiago Motta ameiongoza klabu ya Bologna kwa mafanikio makubwa tangu akabidhiwe timu hiyo mwaka 2022, Hivo kwa miaka miwili aliyokuwepo klabuni hapo ameiwezesha klabu ya Bologna kufuzu ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao ikiwa ni baada ya zaidi ya miaka 50 jambo ambalo limewavutia Juventus na kuona ni moja ya makocha ambao wanaweza kuifikisha timu hiyo mbali.

Acha ujumbe