Tonali Ajipa Matumaini Leao Kubakia Klabuni Hapo

Kiungo wa klabu ya Ac Milan Sandro Tonali amejipa matumaini kua winga matata wa klabu hiyo Rafael Leao raia wa kimataifa wa Ureno ataendelea kusalia klabuni hapo.

Winga huyo ambaye amekua akihusishwa na vilabu vingi barani ulaya kwa siku za hivi karibuni na hiyo ni kutokana na uwezo ambao amekua akiuonesha ndani ya klabu ya Milan, Lakini kiungo Sandro Tonali anaamini mchezaji mwenzake huyo atasalia klabuni hapo.tonaliKlabu ya Ac Milan leo imefanikiwa kupata ushindi katika mchezo wa ligi kuu ya nchini huko baada ya kuifunga klabu klabu ya Salernitana kwa mabao mawili kwa moja, Magoli ya Milan yakifungwa na Sandro Tonali pamoja Rafael Leao.

Sandro Tonali amezungumza na wanahabari baada ya mchezo huo na kumuongelea Leao akisema “Daima amekua kwenye mradi huu wa Milan na hafikirii kuhusu uhamisho, Yeye ni mchezaji wa Milan na anafikiri kubaki hapa tuliona hilo alipofunga bao tunahitaji kumuweka karibu na kumpenda”tonaliWinga Rafael Leao amekua moja ya nguzo muhimu ndani ya klabu ya Ac Milan chini ya kocha Stefano Pioli akifanikiwa kuhusika kwenye mabao mengi ya klabu hiyo, Mchezaji huyo alikua mchezaji bora wa ligi hiyo msimu uliomalizika na kuisaidia Milan kuas mabingwa wa Italia.

Acha ujumbe