Roberto Calenda, wakala wa Victor Osimhen, amewasili katika kambi ya mazoezi ya Napoli ya majira ya joto huko Castel Di Sangro kufanya mazungumzo na wawakilishi wa klabu hiyo juu ya kumuongezea mkataba mteja wake.
Napoli tayari wamekuwa na mawasiliano ya karibu na Calenda majira yote ya kiangazi, kwani wana matumaini ya kumshikilia mfungaji bora huyo bora wa Serie A 2022-23 kwa muda mrefu iwezekanavyo.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Kwanza, kulikuwa na majadiliano wakati timu ilikuwa mjini Dimaro mapema kabla ya msimu mpya, na sasa, kama ilivyoripotiwa na Gianluca Di Marzio, kutakuwa na duru mpya ya mazungumzo.
Vilabu mbalimbali vikubwa barani Ulaya vilihusishwa kutaka kumsajili Osimhen msimu huu wa joto, vikiwemo vilabu vya Chelsea, Manchester United na Paris Saint-Germain, ingawa Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis ameendelea kusisitiza kwamba anataka kumbakisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria huko Naples.
Kwa hakika, ADL ilikuwa imesisitiza kwamba itachukua ofa ya zaidi ya €150m ili kupata usikivu wa Napoli.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.
Osimhen kwa sasa ana kandarasi na Napoli hadi msimu wa joto wa 2025, ambapo kwa sasa anapokea takriban €4.5m kwa msimu.
La Gazzetta dello Sport iliripoti mapema wiki kwamba Napoli iko tayari kutoa mkataba mpya wenye thamani ya kati ya €7m na €7.5m kila mwaka. Di Marzio anaripoti kwamba pande zote zingependa Osimhen abaki na Napoli.