Zaniolo Ajiunga na Atalanta

Mshambuliaji wa kimataifa wa Italia ambaye alikua anakipiga ndani ya klabu ya Aston Villa Nicolo Zaniolo amefanikiwa kujiunga na klabu ya Atalanta kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Zaniolo amejiunga kwa mkopo Atalanta kutoka klabu ya Galatasaray ambapo msimu uliomalizika alicheza kwa mkopo pia klabu ya Aston Villa ya Uingereza, Lakini kwasasa amejiunga na Atalanta kwa mkopo wenye thamani ya €6.4 milioni.ZanioloKlabu ya Galatasaray imeweka kipengele cha €15.5 milioni kwa klabu ambayo itahitaji kumnunua mchezaji huyo, Hivo klabu ya Atalanta kama itahitaji kumpata Zaniolo itapaswa kulipa kiasi hicho cha pesa ambacho klabu ya Galatasaray imekiweka kwenye mkataba wa mchezaji huyo.

Mshambuliaji Nicolo Zaniolo hakua na wakati mzuri sana ndani ya klabu ya Aston Villa kwakua hakua anapata nafasi ya kuanza mara kwa mara kwenye kikosi hicho, Ikielezwa ndio sababu kubwa ya kutimkia Atalabta kwakua anahitaji nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Acha ujumbe