Lengendari wa AC Milan, Zvonimir Boban anaamini Juventus ndiyo wataweza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya -UCL kufuatia ubora wanaouonyesha Serie A.
Juventus wamekuwa wakifanya vizuri kwenye ligi yao ya Italia Serie A, lakini hawajawahi kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya tokea mwaka 1996 na hivi karibuni walipoteza kwenye fainali 2.
Legendari huyu anadai anatambua klabu hii itapitia shughuli pevu kupambana na klabu zingine bora duniani lakini wataenda vizuri. Anaamini uwepo wa Cristiano Ronaldo unamchango mkubwa na kuwaweka karibu zaidi na ubingwa kwa asilimia 15.
Maneno ya Boban Juve kutwaa ubingwa UCL
“NAfikiri kwa walichokionesha, wao ndio timu bora kuchukua ubingwa, japokuwa tunahitaji kuona namna watakavyocheza na klabu zingine bora zaidi”
“Bila shaka wakiwa na Ronaldo timu imekuwa bora kuliko mwaka jana. Ni ngumu kusema ni asilimia ngapi, lakini ni kama anaongeza asilimia 15 zaidi za ubora [Wa Juventus].
Akimzungumzia [Ronaldo] hufunga mara zote, yupo makini sana na huwa mahali anapotakiwa kuwepo kwa wakati muafaka.
Furahav
Juve wako vizuri siku zote.