Juventus Ndio Watapata Ubingwa Ulaya?

Watabe kutoka Italia Juventus wamekuwa wakikimbiza sana msimu huu kuanzia Serie A hadi Ligi ya Mabingwa Ulaya. Juventus wameweza kumpa tabu Manchester United akiwa kwake kwa kukubali kuchapwa bao 0-1. Kuna swali kama kwa mienendo ya klabu hizi mbili ni yupi yupo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuutwaa ubingwa.

Uchambuzi ulioripotiwa na kituo cha habari za michezo cha BBC Sports unaonyesha kuwa klabu ya Juventus kwa sasa imekamilika zaidi ukifananisha na Man Utd hasa katika kipengele cha ubora wa kiufundi kwa nafasi za wachezaji uwanjani ukifananisha na United hivyo wanayo nafasi kubwa zaidi ya kupata Ubingwa.

Juve Ndio Watapata Ubingwa Ulaya?
Kikosi kilichomchapa Man U

Kwa Upande wa Juventus, kuangalia kuanzia kwa golikipa, safu ya ulinzi, viungo mpaka kwa washambuliaji tunapomkuta Ronaldo na Dyabala kikosi hiki kina ubora zaidi unaowafanya wawe na uwezo wa kucheza na kuwachapa timu yeyote wanayokutana nayo.

Uchambuzi huu pia unawaona United kama wamepungukiwa ubora wa kiufundi katika kikosi chake kwa kuwa vitu kama morali na ushirikiano wachezaji wake wanavyo na wanajitahidi zaidi kila wanapocheza wafanye vizuri lakini jitihada zao mara kadhaa zimekuwa haziwapi matokeo wanayotarajia.

Juve Ndio Watapata Ubingwa Ulaya?
Kikosi kilichochapwa na Juventus

Uchambuzi huu hauhitimishi kuwa Man United haina wachezaji bora, hapana, United ina wachezaji wazuri lakini kwa ujumla kama timu wana upungufu katika ubora wao kiufundi. Ukifananisha mafanikio ya Juventus wakiwa nafasi ya 1 na kushinda gemu zao 8 katika 9 wakati 1 wakitoa sare dhidi ya United ambao wako nafasi ya 10 wakiwa wameshinda gemu 4 tu, wametoa sare 2 na kupoteza 3 unaona tofauti kubwa kati yao.

Mabingwa kutoka Italia ndiyo wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kufanya vizuri zaidi na kuchukua ubingwa ukifananisha na United na daadhi ya timu zingine za Ulaya.

2 Komentara

    Juventus watawala seria A now

    Jibu

    Juventus wako vizuri sana

    Jibu

Acha ujumbe