Staa wa Ureno, Cristiano Ronaldo amesaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Juventus ya huko Italia ambapo dau lake ni la dunia nzima!
Mwanzo kabisa dau kubwa la fedha lenye thamani ya paundi milioni 105 lilitajwa kumtoa Ronaldo pale Real Madrid baada ya kuichezea kwa mafanikio makubwa tangu ajiunge nayo akitokea Manchester United miaka kadhaa nyuma.
Kwanini aondoke?
Kuondoka kwake kunakuja baada ya makubaliano ya viongozi wa pande zote mbili pamoja na yeye aliyeomba kutimka klabuni hapo ili akabadili mazingira na pengine kumalizia maisha yake ya kabumbu kule Italia.
Tukio la kushindwa kukubaliana na rais wa Real Madrid, Fiorentino Perez juu ya kuongeza mkataba na Ronaldo yamechangia sana mchezaji huyo kuamua kutimka klabuni hapo kwa dau kubwa alilokuwa akilitaka yeye.
Pia, imesemekana kwamba tetesi za ujio wa Neymar kwa klabu ya Real Madrid ni moja ya sababu za staa huyo kuondoka kwenda kwingine.
Povel
Habar njema