Kabasele Huru Baada ya Rufaa

Rufaa ya Waford kuhusu kadi nyekundu aliyoipata Christian Kabasele katika kombe la ligi kwenye gemu dhidi ya Tottenham Jumatano imefanikiwa.

Staa huyu alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 81, gemu ambayo walichapwa kwenye penati bao 4-2 baada ya kutoka sare ya bao 2-2 kwenye dimba la MK. Sababu ya kadi hiyo ilikuwa ni rafu ambayo alidaiwa kumchezea Dele Alli.

Kabasele alitakiwa atumikie adhabu ya kukosa gemu moja inayofuata ya timu yake lakini adhabu hiyo imefutwa baada ya kufanikiwa katika rufaa yao dhidi ya kadi hiyo.

Taarifa kutoka shirikisho la soka –FA imedai adhabu ya nyota huyu haikuwa sawa na hivyo adhabu yake imefutwa haraka. Kwa sasa nyota huyu ataweza kucheza gemu dhidi ya Arsenal kwenye Ligi kuu kesho Jumamosi.

2 Komentara

    Ni safi tu

    Jibu

    Kabasela mwamba

    Jibu

Acha ujumbe