Manchester City wanakutana na kibarua kigumu wakiwa wanasaka kulinda ubingwa wao EPL. Baada ya kudorora katika gemu kadhaa zilizopita, wamerejea kileleni kwa tofauti ya magoli dhidi ya Livepool walioshuka nafasi ya pili. Manchester City atamkaribisha Chelsea jumapili, gemu ambayo itakuwa ngumu Chelsea wakihitaji kujiimarisha kwenye nafasi yao na kusaka kwenda juu zaidi.
Manchester City anahitaji kupata ushindi dhidi ya Chelsea ili kujihakikishia kuwa anaendelea kuishikilia nafasi hiyo, ushindi tu hautatosha kama Liverpool naye atashinda gemu yake dhidi ya Bournemouth. Man City bado atategemea magoli kuendelea kuwepo kileleni au zaidi amuombee njaa Liverpool ashindwe au atoe sale, kitu ambacho ni kigumu sana kwa Liverpool ya sasa.
Gemu zao 6 za Mwisho (W-Walizoshinda, Walizopoteza)
Man City: WWWLWW
Chelsea: WLWWLW
Uso kwa Uso
Chelsea 2 – 0 Man City , Premier League, December 2018
Chelsea 0 – 2 Man City, Community Shield, August 2018
Man City 1 – 0 Chelsea, Premier League, March 2018
Chelsea 0 – 1 Man City, Premier League, September 2017
Chelsea 2 -1 Man City, Premier League, April 2017
Nani Wanatarajiwa Kuzama Dimbani Jumapili?
Man City: Ederson, Walker, Otamendi, Laporte, Danilo, De Bruyne, Fernandinho, D. Silva, Sterling, Aguero, Sane
Chelsea: Kepa, Azpilicueta, Luiz, Rudiger, Alonso, Jorginho, Kante, Kovacic, Willian, Higuain, Hazard
Zeiyana
Bonge la gemu