Mwandishi wa vitabu C.S.LEWIS amewahi sema kitu kuhusu kiburi “ Kiburi kamwe hakifurahii kuwa na kitu, ila kinapenda kuwa na kitu zaidi ya mwingine, kulinganishwa kunakufanya ujione mkubwa na ujivune, raha huwa juu zaidii ya wengine lakini pindi panakua hakuna mshindani hakuna haja ya kiburi ”

Heshima ndio kila kitu katika maisha hasa katika kazi nenda kila sehemu fanya vurugu utakavyo lakini heshima kwenye kazi ndio kila kitu, hakuna mafanikio bila heshima siku zote utovu wa nidhamu ni zaidi ya kua mlemavu, hata uwe na kipaji kiasi gani na hata uwe na uwezo mkubwa vipi lakini bila hata heshima ya kuigiza huwezi pata kitu.
Mario Baloelli ni kama mvuta bangi yaani akili zake anazijua mwenyewe, matukio yake ya utovu wa nidhamu yameharibu maisha yake ya kimpira na sasa ni kama mwanaume suruali.
Tokea yupo timu za vijana Mario alionekana ni kiapji cha hatari kinakuja japo alifeli majaribio kujiunga na Fc Barcelona , kikubwa Baloteli hana nidhamu ila ni fundi sana.
Roberto Mancini pengine huyu ndo mwanadamu pekee anayeweza kumvumilia Mario yaani anaweza kutukanwa au kukunjwa wakiwa mazoezini lakini akamsamehe, msimu wake wa kwanza seria “A” aliibuliwa na Roberto Mancini kabla ya kuangukia mikononi mwa Mourinho, Mario akiachana na ujinga wake wote kama alivosema Javier Zanetti hii ni aina ya Mourinho, hii ni style ya Jose lakini walishindwana hakuna anayeweza vumilia utukutu..
Mario aliwahi sema baada ya kuchukua tuzo ya kijana mwenye kipaji ( GOLDEN BOY AWARD ) kwamba yeye ndio mchezaji mwenye kipaji zaidii ukimtoa Messi, hapa Balloteli alipita na kauli ya Lewis alikua na kiburi na alipata mshindani alijiona yupo juu sana sana ukumitoa Messi ndio tabia ya kiburi, hii ni dalili mbaya , Ronaldo na Messi wanashinda tuzo hizi kila kukicha lakini hawatoi speech mbovu kama hizi.

Pale Man City Roberto Mancin aliwahi sema utoto unamsumbua sana Baloteli na ni kijana mzuri sanaa mpaka alipokunjwa mazoezini ndio alielewa kwamba jamaa anavuta bangi, akiwa na Man city alikosa zaidii ya mechi 11 za ndani na moja ya nje, akili yake ilimtuma aandike ujumbe kwenye fulana ya ndani na kuandika WHY ALWAYS ME baada ya kuwafunga Man united, Roberto Mancini alishindwa akaamua amrejeshe Italy kwa manufaa yake binafsi , bangi zake zilimtuma afanye matukio mengi ndani na nje ya uwanja..
Mario moyoni anajua kabisa duniani anazidiwa na Messi tu mengine hayajui, baada ya kurudi Milan kule alitulia na alicheza mpira hali iliyowavutia maboss wa Livrpool kumsajili tena , inahesabika ni moja ya usajili mbovu Liverpool kuwahi kufanya mashabiki walifanya kitendo ambacho ni nadra sanaa walirudisha jezi yake madukani , hakuna kocha aliyependa kufanya kazi na Mario Ballotelli mwisho wa msimu alirudishwa kwao Italy , Jurgen Klopp hakutaka hata kumsikia alimuondoa moja moja bila hata kujiuliza..
Hakuna mtu aliyekua na mwisho wa Mario kama alivosema Lewis ukikosa mshindani kiburi hakina namna wala hakina haja kuwepo , kila mtu alimpotezea Mario licha ya kipaji cha kutisha rekodi ya kufunga kwa kila timu anayokwenda lakini hakuna anayepnda bangi zake, moja ya wachezaji viungo wahuni Patrick Vieira baada ya kusaini kuifundisha Nice aliweka wazi hawezi fanya kazi Mario sasa mpaka wahuni wenzake wanamkataa hii ni hatari.
Nidhamu ya Mario imemuharibia maisha kimpira amechoka mapema na sasa ni kama mwanaume suruali ,kiburi kinakua kizuri hadi awepo mtu wa kushindana nae watu wameamua kumpotezea hawana time nae, nje ya big six Mario anacheza uhakika pale EPL lakini hakuna wa kufanya nae kazi…
Mario angekua serious na kazi yake huku nje watu wasingehusika hata kidogo. Zlatan Ibrahimovic ni mwehu sana lakini ikifika kazini anakuwa zaidi ya serious Sergio Ramos akili zake anazijua mwenyewe lakini ndani ya uwanja hawezi pigana na mchezaji mwenzake. Vinnie Jones alikua gaidi kwenye kazi ila hakua mpumbavu.
Hristo Stochkov alikua zaidi ya mwehu lakini mwaka 1994 alichukua Ballon D’or. Kuna wachezaji waengi wavuta bangi kama Mario Balotelli lakini walikua hawachelewi mazoezini walikua hawapigani na makocha wao walikua na akili ya kumdhuru mpinzani kimatokeo.
Sasa yupo zake kule Brescia timu isiyo na uhakika wa kubaki ligi kuu , kawa Hovyo hata raisi wao hamtaki…
imeandikwa na EZEKIA JOHN KANDONGA



Zeiyana iddi
Sifa sio nzuri..!
Emmy cleopa
Heshima ndio kila kitu kiburi si kitu kinzur
Sasa utajifuza kulingana na kosa
Frank patrick
Black arafu tajiri arafu maarufu afanyaje sasa🤗🤗
Neema hassan
Kama hakutokuwa na timu kubwa itakayomsajl kwa kpnd hk..atajifunza kulingana na makosa yake.
Hopemwaikux
Jeur yake ndo inamponza hata simuelewag huyu mtu
Salma
Hakuna kitu kizuri kwe maisha kama heshima
Zainabu
Ukiwa na heshima bx utakua na mashabiki wengi
Theckla
Kiburi si uungwana
Mwanaidi
Anatakiwa kuomba radhi kwa uongozi wa timu laa sivoo itamuwekea rekodi mbaya
Gabriel
Kwel ital ilikuwa na ubaguz xo kupatikana na black balotel na kuonekana anakipaji ndo mambo yakawa hvyo but hana kibur kihivyo
Tahiya
Kubaguliwa kwa wachezaji wenye ngozi nyeusi ndio kunasababisha baadhi ya wachezaji kuwa na viburi
Fatina
Heshima inamfanya m2 afike mbali kwenye maisha
mathayo sonje
watu wengi hawamuelewi balotili ndio maana anaonekana kama kibuli ila anasimamia anachokiamini
frank
baloteli ana utoto mwingi sana cjui ata kua lini uyu jamaaa
Mariam
Duuuh
Mwanahamisi
Heshima ni kitu Cha bure
Devotha
Baloteli acha kiburi jaribu kukua ili upate heshima ya kustaafu
Genia Sikaluzwe
Hakuna kitu kizuri kwenye maisha Kama heshima