Klopp Awaomba Radhi Mashabiki

Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo baada ya kupoteza mchezo wa robo fainali wa michuano ya Europa League usiku wa jana.

Klabu ya Liverpool jana walipokea kipigo cha mabao matatu kwa bila katika uwanja wao wa nyumbani kutoka kwa klabu ya Atalanta, Jambo ambalo limemfanya kocha Klopp kuomba radhi kwa mashabiki wa klabu hiyo.klopp“Tunapaswa kuonesha mabadiliko kwa asilimia 100, Jambo ambalo nina uhakika nalo, Nitafikiria jambo hili, Hii sio mara ya kwanza kupoteza mchezo kwa bahati mbaya kama hivi, Lakini tutaonesha mabadiliko naahidi hilo”

Kocha huyo amewapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kua watakwenda kufanya mabadiliko makubwa katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Alhamisi ya wiki ijayo nchini Italia katika dimba la Gewiss ambao ni uwanja wa nyumbani wa Atalanta.kloppKocha Jurgen Klopp ana matumaini hayao kwani sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo kupoteza mchezo wa kwanza katika hatua za mtoano na kupindua meza katika mchezo wa pili, Hii ndio sababu kubwa ambayo imemfanya kocha huyo kutoa ahadi kwa mashabiki wa klabu hiyo kwani ni kawaida ya klabu hiyo kupindua meza.

Acha ujumbe