Ilikuwa tarehe 20 Julai 2004, katika viunga vya jiji la London, mitaa ya Fulham uliopo uwanja wa ndege wa Heathrow. Alishuka mreno Jose Mourinho na ndege ya kukodi kutoka Ufaransa, pembeni yake alikuwepo kijana mmoja asiyefahamika kutoka pwani ya Afrika, Cote d’Ivoire.

Waandishi walioshinda uwanja wa ndege mchana kutwa kumsubiri Mourinho, walimuwahi kuihoji safari yake ya kwenda Ufaransa. Mou hakujishughulisha kuongea naò, aliunyanyua tu mkono wake kumuelekea Drogba, akiwaeleza kwa ishara kuwa huyu ndiye niliyemfuata Marseille. Wengi walishtushwa na usajili ule usiyotarajiwa.

Hadi tajiri Roman Abramovich alisita kulipa pesa ili kuipata saini ya Didier Drogba. Pauni milion 24 kwa mchezaji ambaye hajafanya lolote la kutisha akiwa na miaka 26? Ilikuwa ngumu, ila Mourinho alishikilia msimamo kuwa ili ashinde mataji, anamuhitaji Didier Drogba. Dunia ilimshangaa, unamng’ang’ania vipi huyu mvulana kwenye dunia yenye Thierry Henry, Samuel Eto’o na Andriy Shevchenko?

Ila dili lilikamilika na kila mtu anajua nini kilifuata baada ya hapo. Drogba aliitendea haki kila pasi ya Frank Lampard, mitungi ya Ashley Cole na Majaro ya Alex Rodrigo. Misimu tisa aliyoikaa darajani, amepiga mabao 164, amechukua premier league 4 na FA Cup 4 pale. Ameipa Chelsea UEFA 2012. Ukimtaja ‘legend’ mmoja wa Chelsea leo. Jina lake litakuwa ‘Didier Drogba’.

Samahani mashabiki wa Chelsea kwa kuwachelewesha, ila tuujadili ujio wa Timo Werner. Yeye anakuja akiwa ameshaiaminisha dunia uwezo wake. Msimu huu pekee ameshawafungia RB Leipzig mabao 32 na ‘ku-assist’ mengine 13 katika michezo 43. Unyama ulioje kwa kijana wa miaka 24 tu.

Ameweka rekodi nyingi tu pale Bundesliga. Mchezaji mdogo zaidi kuwahi kufunga mabao mawili katika Bundesliga, mchezaji mdogo zaidi kuwahi kucheza michezo 200, mabao yake 21 yakaipeleka Leipzig UEFA kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yao. Binadamu wa kwanza kuipa Leipzig ushindi mbele ya Bayern Munich.

48 MAONI

  1. mzee unamjua drogba lakini dunian alikuwepo drogba mmoja tu kutokea ivory cost hatokuja kutokea yule tena maana mama yake drogba alisha maliza kazi

  2. Ni tofaut kati ya didier drogba na timo werner .timo tayar ana umri ndogo tayar kasha tengeneza rekodi basi msimu ujao utakua na uahindan mkubwa sana

  3. Hatuwezi kuthibitisha hill kwa maneno au kwa mtazamo ingawa uwezo wa Tim Werner tunaufahamu akiwa na timu yake ya zamani Rb Leipzig kwamba ni mkubwa Sana ila haidhihilishi kabisa kwamba ni drogba mpya kwa sababu tumeshuhudia hili wachezaji kibao waliokuja pale darajani na kufananishwa na drogba au mrithi wake na wakachemka mfano lukaku alikuja darajani kwa kuchukua nafasi ya drogba ila mwisho wa siku ikaonekana hajamudu kuchukua nafasi hiyo ya mchezaji wa taifa ya cote d’ivoire didie drogba wengi tunafahamu mambo aliyo yafanya drogba akiwa na timu ya Chelsea ni makubwa na hayasauliki katika vichwa vya wana Chelsea kwaiyo hatuwezi kuthibitisha hill kwa kuangalia uwezo wake aliokua nao time Werner akitokea rb Leipzig ila tunachoomba wana Chelsea Tim Werner aendane na falsafa ya Chelsea na tunatarajia kuona performance yake nzuri akiwa chini ya kocha Frank lampad hapo ndipo tutathibitisha kwamba huyu sasa ndie drogba mpya ila kwa sasa ni vigumu kuwaaminisha wana chelsea kua Werner ndie super drogba mpya wa Chelsea.

  4. Kila mtu amepewa talanta yake sio rahisi na haijawahi kuwa rahisi talanta ya Drogba ikafanana na mwingine achilia mbali Timo. Tusubiri kuona mavituzi yake Darajani#meridianbettz

  5. Ni bado kwa werner kuwa drogba mpya ajafikia levo hizo drogba ni streika mwingine chelsea na legend alieacha alama the blues

  6. Hatuwezi kuthibitisha hill kwa maneno au kwa mtazamo ingawa uwezo wa Tim Werner tunaufahamu akiwa na timu yake ya zamani Rb Leipzig kwamba ni mkubwa Sana ila haidhihilishi kabisa kwamba ni drogba mpya kwa sababu tumeshuhudia hili wachezaji kibao waliokuja pale darajani na sio kufananishwa na drogba

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa