Kushangilia Kumemponza Spalletti Gemu 1

Kocha wa Inter Milan, Luciano Spalletti atatakiwa kusimuliwa tuu yatakayojili uwanjani baada ya kupata adhabu ya kutohudhuria gemu moja.

Spalletti amepata adhabu hii baada ya kushangilia sana mbele ya kamera akitafsiriwa kumshambulia muamuzi msaidizi ambaye alikuwa karibu na mpiga picha aliyekuwa na kamera hiyo.

Kocha huyu alishangilia kwa sauti akiitazama kamera kuonyesha furaha yake baada ya kupata goli katika dakika za mwisho kabisa 90+3 ambalo liliwapa ushindi wa 1-0 dhidi ya Sampodoria Jumamosi.

Spalletti ataikosa gemu dhidi ya Fiorentina kesho Jumanne Septemba 25, kosa lake anadaiwa ni β€˜kumshambulia muamuzi msaidizi’ kwa kupiga kelele za shangwe mbele yake.

Lakini baadhi ya wakosoaji wanadai kuwa Spalletti hakustahili adhabu hiyo kwa sababu yeye hakuwa amemlenga muamuzi msaidizi kama inavyodaiwa, yeye alimlenga mpiga picha ili aonekane kwa mzuka aliokuwa nao.

Acha ujumbe