Kila mtu huwa na kipindi fulani kigumu anachokipitia au alichokipitia ambacho hataweza kukisahau kabisa. Mwanadada nyota wa tenisi Petra Kvitova naye amezungumzia kumbukumbu yake kuelekea fainali za michuano ya Australian Open.

Mwanadada huyu anasema kuwa anakumbuka alivyoumizwa vibaya baada ya kupambana na mtu aliyemvamua na kisu mwaka 2016, alipata majeraha kadhaa ambayo watu wengi walivyomtazama hawakuwa na tumaini kuwa nyota huyu angeweza kurejea kucheza mchezao wa tenisi.

hata hivyo, mwanadada huyu hakuvunjika moyo, aliamini kuwa angeweza kurejea uywanjani, hakuweza kuruhusu mawazo hasi kuhusu maendeleo yake juu ya uwezekano wake wa kurejea mchezoni japokuwa anasema ilimuwia vigumu sana kuweza kuwaamini watu wa karibu yake hasa wanaume baada ya tukio hilo lililo muacha na maumivu ya mda mrefu.

Australian Open
Amewashangaza wengi akindelea kufanya vyema licha ya ugumu aliouupitia. Kvitova, amemchapa Danielle Collins kwa seti ya 7-6 (7-2) 6-0 leo kufikia fainali za mmoja mmoja za wanawake kule Melbourne.

Mwanadada huyu anatarajia kukutana na bingwa wa US Open Naomi Osaka Jumamosi hii kwenye fainali za michuano hii ya US Open.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa