Lewandowski Kuzifukuzia Rekodi za Muller

Ni mara chache mno msimu wa ligi kuu ujerumani kuisha bila mchezaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski kuweka rekodi kwa timuyake ama kwa nchi kiujumla.na kudhihirishia Umma kua kampeni ya kumchagua kua mchezaji bora namba 9 kwa ulaya haikua ya kimakosa.

Kwenye mchezo wa tisa wa msimu wa 2019-20 Lewandowski alikuwa ndie mchezaji wa kwanza kwenye historia ya Bundersliga kufunga magoli kwenye mechi tisa mfululizo kwa wachezaji wa timu za juu, kwa kufunja rekodi iliyowekwa na Pierre-Emerick Aubameyang.

Lewandowski kushoto akishangilia na Tomas Muller

Kwa magoli 13 ndani ya michezo tisa katika msimu wa 2019-20, Lewandowski alivunja rekodi ya mchezaji asie na Asili ya Ujerumani Aubameyang ya kufunga magoli 31 kwa msimu mmoja na Gerd Muller mkongwe wa ligi hiyo aliye funga magoli 40 kwa msimu wa 1971-72 kwa kipindi chake.

Lewandowski ana njia zake ambazo anaweza kumzidi Muller kwenye rekodi za mfungaji bora wa muda wote wa Bundersliga,kwasasa tofauti yao ni magoli 31 tu na ukizingatia Lewandowski hakucheza mechi zake 10 baada ya kusajiliwa mwaka 2014 lakini kwa sasaΒ  bado ana muda mrefu wa kuendelea kucheza na kufunga magoli.

Yatazame hapa magoli 5 bora ya Robert Lewandowski kwa msimu wa 2019-20

 

Cha zaidi mpaka hivi sasa uwezo wake unaridhisha na ukizingatia amesha funga magoli 13 ikifuatiwa na magoli ya misimu kadhaa iliyopita ambayo nayo yanapelekea Lewandowski kuikaribia rekodi ya Muller.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.