Sir Lewis Hamilton na Serena Williams wanaripotiwa kuweka £20m kwenye dau la Sir Martin Broughton kuinunua Chelsea.

Muungano unaoongozwa na mwenyekiti wa zamani wa Liverpool Broughton, ambaye ni mojawapo ya mapendekezo matatu yaliyosalia katika mbio za kuwanunua wababe hao wa Premier League katika wiki zijazo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Sky News, zabuni hiyo imepata msukumo wa hali ya juu huku kila mmoja, Hamilton na Serena Williams akiwa tayari kufadhili ofa hiyo.

Ripoti hiyo inadai kuwa Hamilton, bingwa wa dunia wa mara saba kwenye Formula 1, na mcheza tenisi Serena Williams wako tayari kuwekeza £10m kila mmoja katika mradi huo unaopendekezwa.

Aidha, inadaiwa kuwa majadiliano baina ya pande husika yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadhaa, huku uamuzi huo ukielezwa kuwa ni uamuzi mzito wa uwekezaji.

Benki ya wafanyabiashara ya Marekani ya Raine Group inatarajiwa kufanya uamuzi zaidi kuhusu mchakato kukamilisha ununuzi huo kwa wakati ufaao, huku miungano ya wanunuzi ikiongozwa na Todd Boehly na Stephen Pagliuca na wagombea wengine wawili waliopo katika kinyang’anyiro hicho.

Sir Lewis Aungana na Serena Williams Mpango Kuinunua Chelsea!
Lewis Hamilton na Serena Williams wanahusishwa na dili la kuinunua Chelsea.

VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa