Liverpool Na Jaribio la Mwisho kwa Isak

Muda unazidi kuyoyoma kwa Alexander Isak kutimiza ndoto ya kujiunga na Liverpool. Klabu hiyo imekuwa ikimvutia kwa muda mrefu na tayari walishatoa ofa ya pauni milioni 110 mapema dirisha hili la usajili, ambayo Newcastle waliikataa.

Isak amekuwa moja ya hadithi kubwa za usajili msimu huu baada ya kuwajulisha Newcastle kwamba anatamani kutafuta changamoto nyingine. Hata hivyo, klabu hiyo ya Tyneside imeendelea kusisitiza msimamo wao kwamba nyota huyo wa Sweden “hauzwi.”

Liverpool Na Jaribio la Mwisho kwa Isak

Kwa mujibu wa BBC Sport, Liverpool wanajiandaa kufanya “jaribio la mwisho” la kumsajili Isak kabla ya muda wa mwisho Jumatatu saa 1 usiku.

Inadaiwa kuwa Newcastle bado wanahitaji kusajili washambuliaji wawili kabla ya kumruhusu Isak kuondoka. Wamekuwa wakimfuatilia Nick Woltemade kutoka Stuttgart, Jorgen Strand Larsen wa Wolves na Yoane Wissa kutoka Brentford. Ikiwa mmoja wao ataingia kwenye kikosi cha Eddie Howe, basi inaweza kufungua milango kwa mabingwa hao wa EPL kuwasilisha ofa mpya kwa Isak.

Lakini kwa hali ilivyo sasa, ili kupata nafasi yoyote ya mafanikio, Liverpool huenda wakalazimika kutoa zaidi ya pauni milioni 120.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Liverpool Na Jaribio la Mwisho kwa Isak

Wakati huohuo, Football Insider inaripoti kuwa Liverpool wanamwangalia Morgan Rogers endapo RB Leipzig watawasilisha dau linalolingana na thamani ya Harvey Elliott. Hata hivyo, Liverpool ECHO inaeleza kuwa The Reds hawatakuwa tayari kuachia kiungo huyo kirahisi.

Klabu ya Bundesliga hiyo imekuwa kwenye mazungumzo na Liverpool kuhusu Elliott kutokana na hali ya sintofahamu ya mustakabali wa Xavi Simons. Lakini baada ya Simons kujiunga na Tottenham, matarajio ya Leipzig kumvizia Elliott yanatarajiwa kuongezeka zaidi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.