Luka Jovic Kukoswa na Liverpool

Liverpool watakuwa wanajiandaa kumkosa mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Luka Jovic msimu huu wa joto wakati Real Madrid wakionekana wanaweza kuinasa sahihi yake.

Nyota huyu wa miaka 21 amekuwa akivutia vilabu vikubwa kwa kazi yake anayoichapa kule Bundasliga, tokea alipojiunga Eintracht Frankfurt akitokea Benfica mwaka 2017.

Liverpool wamekuwa wakimfuatilia staa huyu lakini Real Madrid ndio wanaoongoza mbio za kumnasa Luka Jovic wakiwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuinasa sahihi yake.

Mkurugenzi wa Eintracht Frankfurt Fredi Bobic anasema kuwa kuna uwezekano zaidi nyota huyu akamwaga wino kwa Real Madrid.

“Ninatumaini nahitaji abaki hapa Eintracht, lakini najua ni wazi kuwa klabu kubwa kama Real Madrid wanamuhitaji na wapo kwenye nafasi nzuri ya kumchukua.”

Staa huyu ame amechaoa magoli 17 kwenye Bundasliga msimu huu na kuonesha jitihada zake kwenye ligi ya Europa akiweka wavuni magoli 8 kuwasaidia timu yake kuingia nusu fainali watakapo kutana na Chelsea.

3 Komentara

    Duuh hatari sana

    Jibu

    Noma sana

    Jibu

    Jovic yuko vizuri.

    Jibu

Acha ujumbe