Maguire Atolewa kwenye Kikosi cha Uingereza

Nahodha wa Manchester United na beki wa timu ya taifa ya Uingereza – [Harry] Maguire, ameondolewa kwenye kikosi cha Uingereza muda mfupi baada ya kupatikana na hatia ya makosa aliyoshitakiwa nchini Ugiriki.

Mapema wiki iliyopita, Maguire alishitakiwa kwa makosa ya kumtukana na kumpiga afisa wa polisi pamoja na vitendo vya rushwa wakati akiwa likizo pamoja na rafiki zake nchini Ugiriki.

Taarifa ziliripoti vitendo hivyo vilitokea baada ya mtu mmoja kumchokoza dada yake Harry na hivyo vurugu za maneno na vitendo kutokea katika visiwa vya Mykonos. Mapema siku ya Jumanne, wakili wa beki huyo alikanusha mashtaka hayo.

Jumanne jioni ilitoka taarifa ya Harry kuhukumiwa miezi 21 jela na hivyo kocha wa Uingereza kuchukua uamuzi wa kumuondoa beki huyo kwenye kikosi chake.

Maguire kukosekana kwenye Kikosi cha Uingereza.

“Kutokana na taarifa za hivi punde, ninathibitisha kumuondoa Maguire kwenye kikosi cha Uingereza kitakachocheza michezo dhidi ya Iceland na Denmark.

“Kama nilivyosema mwanzoni, nilikuwa ninaliangalia jambo hili linavyokwenda. Baada ya kuzungumza na Manchester United pamoja na mchezaji mwenyewe, nimefikia uamuzi wa kumuondoa Harry Maguire kwenye kikosi kwa maridhiano ya pande zote na kwa ajili ya maandalizi kuelekea michezo hiyo.” amesema Kocha wa Uingereza – Gareth Southgate.


Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

40 Komentara

    Nidhamu nj muhimu sana katika mchezo na jamii inayokuzunguka sheria ifuate mkondo wake pale wanapofanya kosa

    Jibu

    maguire anaweza kushuka kiwangona thamani yake kibiasha anatakiwa ajilekebishe atari sana hiii upande wake

    Jibu

    Nidhamu Ni kitu muhimu sana ktk jamii inayokuzunguka na popote unapokuwa@meridianbettz

    Jibu

    Nidhamu ni Jambo muhimu sana katika wachezaji

    Jibu

    Nidhamu Ni muhim sana katika michezo shelia ifuate mkondo wake pale wanapofanya kosa#Meridianbettz

    Jibu

    sheria ifate mkondo wake pale panapokuwa na kosa

    Jibu

    Nidhamu Ni Jambo njema kwa Kila mchezaji kwaiyo acha Sheria ifate mkondo wake ili iwe funzo kwa wengine!

    Jibu

    Ni vizuri ajifunze kua na nidhamu

    Jibu

    Maguire alikosa heshima na nidhamu nje ya kazi na ndani ya kazi adhabu aliyopewa anastahili

    Jibu

    Kwa kumuangalia Maguire huwani kabic na kitendo alicho fanya me naona ilikua asila tu daaah…!

    Jibu

    Itakuwa fundisho kwa wachezaji wengine

    Jibu

    Wamefanya vizuri wakimuongezea na adhabu nyingine ili iwe fundisho kwa wengine

    Jibu

    England watakua na pigo kubwa kwa kukosekana kwa Maguire kwani kwa sasa ni kiongozi mkubwa kwenye ngazi ya klabu na Taifa inabidi wakate rufaa ili kesi hyo isikilzwe tena

    Jibu

    itakua fundisho siku nyingine kwake na wengine

    Jibu

    Ni kheri ajifunze nidhamu

    Jibu

    Nidhamu muhimu

    Jibu

    Itakuwa fundisho sana

    Jibu

    Ni vizuri ili ajifunze heshima na ikumbukwe kila mtu nilazima ajue yeye ni nani na kwanini yupo hapa duniani na akitoka hapa duniani ataenda wapi

    Jibu

    Kitendo alichoamua Gareth Southgate kocha wa uingereza kwa kumtoa maguire sio mbaya maana kwanza ameangalia nidhamu ya timu na pia kingemfanya magu asicheze kwa Uhuru maana kwa tukio hilo amefanya kwa hasira

    Jibu

    Waingereza wanakosea kumuacha huyu beki sasa watamuweka nani pale

    Jibu

    Nidhamu ni jambo la msingi sana.

    Jibu

    Sijui nini kimemupata Harry Maguire na nduguze kupigana na polisi na kujaribu kutoa rushwa na mwisho wa siku ameadhibiwa baada ya kupatikana na makosa yote hayo, kwa mtu mwenye jina kubwa kama yeye alipaswa kujizuia#meridianbettz

    Jibu

    Lazima hatua za kisheria zifate mkondo wake

    Jibu

    Parfomance yake haikuwa vizuri msimu ulioisha.

    Jibu

    Maguire anaweza kushuka kiwango na pia anajishusha utu , haikuwa haha ya yye kutakan ni muhimu tu angefanya funika kombe mwanaharamu apite.

    Jibu

    Ilo ni fundisho

    Jibu

    Ndo faida ya kutokua na nidham

    Jibu

    Hili ni funzo kwa wengine!!!

    Jibu

    Sheria imefuata mkondo wake

    Jibu

    Duuh Kweli ni mtovu wa nidhamu haki yake kufukuzwa

    Jibu

    Dah hii issue imemchafua sanaa

    Jibu

    Hakua kwenye wakati mzuri ndani ya club ya man u 2020/2021 sababu hiyo imepelekea asiitwe kwenye kikosi cha uingereza.

    Jibu

    Duu Nini Sasa aundio ukosefu wanidhamu jamani

    Jibu

    Kashfa mbaya sana kwa Maguire

    Jibu

    Majanga

    Jibu

    Nidhamu Ni muhim sana katika michezo shelia ifuate mkondo wake pale wanapofanya kosa

    Jibu

    kosa alilolifanya ni kubwa sana ila kwa sisi mashabiki wa united tunabaki mikono tumeweka katika mashavu

    Jibu

    Dooo pole yake sana

    Jibu

    Balaa zito

    Jibu

    Pole yake iwe funzo na kwawengine

    Jibu

Acha ujumbe