Ni dhahiri, mashabiki wa Man United wamechoshwa na muenendo wa klabu yao kwa miaka ya hivi karibuni. Msimu huu unaweza kuwa donda limeshika hatamu, maumivu ni makali!

Kabla ya msimu huu kuanza, United walitikisa soko la usajili kwa kuwasajili Jadon Sancho, Rafael Varane na Cristiano Ronaldo. Msimu ukaanza, matokeo yakaanza kuwa ni kinyume na kilichotarajiwa, Ole Gunnar Solskjaer akaambulia kufukuzwa na Ralf Rangnick kupewa kazi ya muda.

Ralf huyu hapa, michezo 23 ameshinda michezo 9 pekee. Wenyewe wanakwambia “this is not good enough” ni ukweli, hii sio level ya Man United inayojulikana kwa ubabe wa kutwaa mataji.

Man United
Ralf Rangnick.

Kwa takribani mwezi mzima, stori kubwa ni kocha mpya wa Man United. Hapa ni vita ya Mauricio Pochettino vs Erik Ten Hag. Kati ya hawa, Ten Hag anapewa nafasi kubwa ya kutua Old Trafford akitokea Ajax. Lakini, huu mchongo utatimia au utaungua?

Inaripotiwa kuwa, Ten Hag anaofa mbili mezani kwake – moja inatoka RB Leipzig huku (ofa) nyingine ikiwa ni kule Old Trafford. Pamoja na hili, kuna uwezekano akasaini mkataba mpya na Ajax. Kwa kinachoonekana, huenda mchongo wa United ukaungua na, The Red Devils watakua na kazi ya ziada kumsaka kocha wa muda mrefu.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa