Klabu ya Man united imepata ushindi wake wa kwanza katika ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Liverpool katika dimba lao la nyumbani Old Trafford. Man United ya imepoteza ushindi michezo yake miwili ya awali dhidi ya vilabu vya Brighton pamoja Brentford. Mchezo ambao ulitawaliwa na kasi na mashambulizi ya kupokezana kwa kila upande.

Ni Man United walioanza kupata bao la kuongoza mnamo dakika ya kumi na sita ya mchezo kupitia kwa winga wake hatari Jdon Sancho.

Mpaka mchezo unakwenda mapumziko United walikua mbele kwa bao moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku United wakifanya mabadiliko ya mapema baada ya kutoka winga Antony Elanga na kuingia Anthony Martial.

united, Man United Yafufukia kwa Liverpool., Meridianbet

Haikuchukua mda mrefu kuona madhara ya mabadiliko ya Martial kwani ni yeye aliepiga pasi ya bao kwa Marcus Rashford aliefunga baao dakika ya 53 ya mchezo na United wanapata uongozi tena kwa mara ya pili.

Mwalimu wa Liverpool nae hakua nyuma kwenye kufanya mabadiliko ili kuirudisha timu yake mchezoni baada ya kumuingiza kiungo wa kibrazil Fabinho na kinda mwingine wa kibrazil Fabio Carvallho ambao walikuja kubadilisha mchezo.

Dakika ya 81 ya mchezo Mohamed Salah anbae anaipatia Liverpool bao la kufutia machozi na mchezo unamalizika kwa Liverpool kubanwa mbavu na Manchester United.

Hali hii inawafanya Liverpool kutokushinda michezo mitatu mfululizo ya awali ndani ya ligi kuu ya uingereza baada ya kusuluhu michezo miwili ya mwanzo na jana kuangukia pua dhidi ya Man United. United waliokua wanashika mkia kwenye nafasi ya 20 kwenye ligi wanapanda mpaka nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Tukio lingine lililovuta hisia kwenye huo ni utambulisho wa kiungo mpya wa Man United kutoka Real Madrid ya nchini Hispania katika viunga vya Old Trafford.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa